Moto katika mazingira yanayoshindaniwa-kufanya kazi na washikadau wa Kenya kuelekea mbinu ya udhibiti wa moto iliyoondolewa ukoloni

Moto katika mazingira yanayoshindaniwa-kufanya kazi na washikadau wa Kenya kuelekea mbinu ya udhibiti wa moto iliyoondolewa ukoloni

Muhtasari kutokana na sayansi ya kuondoa ukoloni wa moto-Warsha ya moto kote katika mandhari yaliyogombewa(1-2 disemba,2022, Nairobi), na Adriana Ford na Abigail Crocker.

iliyotafsiriwa na Elijah Praise

[English version here]

 


Katika mahali kwingi ulimwenguni,simulizi za kikoloni za kupambana na moto,kama vile Imani kwamba watu wa kiasili na jumuiya za mitaa huchoma ovyo,yanazidi kueleza mikakati ya uhifadhili.Hasa hii ni kweli katika maeneo ya hifadhi ndani ya mandahri ya moto,ambapo,sera za kuzima moto na kutengwa kwa watu na mifugo zilifafanua upya mifumo ya usimamamizi wa moto na kubadilisha utawala wa moto uliokithiri. Hii inatumika katika kudumisha “kitendawili cha moto wa porini,” ikisababisha kuenea kwa uharibifu wa mfumo wa ikolojia, upotevu wa viumbe hai,na udhaifu wa kijamii-kiuchumi.

Kuendelea Zaidi kwa sera za kuzima moto katika mifumo ya usimamizi wa mazingira duniani kote, hasa katika makoloni ya walowezi na mataifa yaliyotawaliwa na ukoloni wa kihistoria,sit u kuendesha uharibifu wa ikolojia, lakini pia kuwakilisha changamoto za kina zinazohusiana na ukosefu wa haki ya kijamii na kiikolojia,kutiishwa,na utengaji wa maliasili.Hata hivyo, tunajua kwamba watu wakiasili wanajumuisha chini ya 5% ya idadi ya watu duniani ijapokuwa wanasimamia 25% ya uso wa dunia na kulinda Zaidi ya 80% ya bionuwai iliyobaki.Wao ndio wasimamizi wakubwa Zaidi wa mazingira katika sayari.

Tarehe 1 na 2 desemba 2022,watendaji wa maliasili 25,wamiliki wa haki,na watafiti kutoka kote Kenya walikuja Pamoja katika chou kikuu cha Strathmore Nairobi kwa warsha ya kuchunguza njia za kuondoa ukoloni wa usimamizi wa moto n ani nini kinahitajika kusimamia moto katika muktadha wa kenya. Warsha hii ilipangishwa na Leverhulme Wildfires EDI Working Group kama sehemu  yake ya programu ya kuondoa ukoloni katika sayansi ya moto,ikiungana Pamoja na  Centre of Biodiversity Information Development, Strathmore Universitykutokana na msaada wa Grantham Institute – Climate Change and the Environment. Wanachama wa “Leverhulme Wildfires”, waliokuwa wamekutana Pamoja katika Royal Holloway huko London kwa warsha sambamba, waliungana na warsha yenyewe mtandaoni, ikikubalisha kubadilishana kwa mawazo na maarifa kati ya wahusika wa Kenya na UK.

Warsha hii, ambayo,ililenga kuleta mfano rahisi na unaoweza kubadilika na ambao unaweza kutumika kote mbalimbali Pamoja na mazingira yanayogombaniwa, Ilihusisha mbinu mbalimbali za kuchunguza mawazo na mitazamo, Pamoja na picha Tajiri,Café ya dunia,Sanaa shirikishi na video shirikishi, Sanaa inayoishi, mawasilisho,na maendeleo ya tamko la Pamoja. Huku ripoti kamili, itapatikana mapema 2023, itatoa majadiliano na uchambuzi wa kina wa warsha hii,hapa ni kwa kifupi kuhusu mbinu muhimuza kueleza baadhi ya rasilimali na matokeo ambayo yanapatikana mara moja.

 

MOTO UNA MAANA GANI KWAKO?

Baada ya kuanzisha muktadha na usuli ya kuondoa ukoloni wa sayansi ya moto, tulichunguza swali pana ya “moto una maana gani kwako,”tukitumia mbinu ya picha tajiri. Wahusika walikuja Pamoja katika vikundi kuchora jinsi walivyo hisi kilikuwa cha muhimu kuhusu moto,na maana ya moto katika madhari yao, hivyo basi wakajadiliana na kushiriki picha zenyewe kwenye kundi zima. Hii ilidhihirisha mitazamo hasi huathiri moto wa nyika katika mandhari, Pamoja na tishio kwa Wanyamapori, pia vipengele vyema vinavyowekana, kama kuzaliwa upya kwa mimea.

 

Utawala wa Moto

Ili kutafakari kwa undani Zaidi kuhusu utawala wa moto, ikiwa ni Pamoja na usawa na usimamizi wa uondozi wa ukoloni wa moto, tulitumia mbinu ya “Café ya dunia”ambapo washiriki walitoa maoni kwa maswali tofauti ,kusonga kutoka meza kwa meza kuongeza maoni Zaidi kwa yale ambayo tayari yalishirikiwa. Tulichunguza Pamoja maswali ya “Moto usimamiwa vipi katika mandari yako?”, “Ni nini ungependa kubadilisha katika usimamizi wa moto?”, “Ni changamoto gani ambazo zinazuia jumuiya za mitaa katika kujihusisha katika utawala wa moto?”, “Ni nini vizuizi vya kitaifa na kikanda vya usimamizi na utawala wa moto?” (Mf. Kijamii,kiuchumi,kisiasa,kisheria)?”Na mwisho kabisa, “Nini inafaa kufanyika ili kuwezesha usawa katika usimamizi na utawala wa moto?” (Tazama hapa chini).Tulijadili majibu ya wahusika na sababu zao za kujibu vile-kwa mfano, Katika jukumu la miradi ya mikopo ya kaboni katika usimamizi wa moto wa misitu katika mitaa (Mf. REDD+), na utafauti ulioko katika “maarifa ya kitamaduni” kati ya kizazi cha vijana na wazee ndani ya mkutano na jinsi ilivyo athari majibu ya wahusika.

Pia tulitumia njia ya ushirikiano katika zoezi la kuramani uhusiano kati ya wahusika tofauti katika warshi, jukumu zao na vikundi, miradi ambayo wanahusika,wadau wanaofanya kazi nao,na yeyote ambaye alitengwa kutokana na miradi hiyo.

Mapping roles and stakeholders amongst workshop participants

Jukumu la uramani kwa wadau miongoni mwa wahusika katika warshi

 

KUTUMIA SANAA KUTAFAKARI NA KUTOA CHANGAMOTO KWA SIMULIZI ZA MOTO

Tukitambua nguvu na uwezo wa Sanaa katika kutafakari na kutoa changamoto katika simulizi na mawazo na kuunganisha kazi yetu katika Wildfires at the Art-Science Interface, tulimualika msanii Shedrack Musyoki aungane nasi katika warshi. Shedrack ni msanii maarufu ambaye uishi Nakuru nchini Kenya,ambaye kwa mara nyingi utumia michoro kwa kushirikisha kama njia ya kuleta watu Pamoja kusimuliana hadithi. Shedrack awali aliwasilisha uchongaji yenye jina makazi(Kuumanisha nyumbani) kuangazia athari ya moto wa misitu.

Katika asili, na pia warshi ikiendelea (na baadae), alitengeneza vipande vitatu vilivyoagizwa kama sehemu ya mradi-Kipande kilicho hai chenye jina “Mambo leo”(inayo na maana “masuala ya sasa”)akiweka msingi kutoka na Mijadala aliyosikia katika warshi na akaipea jina chaguo ni letu( ikiwa na maana (The choice is ours),na uchongaji wa kuhusisha kwa jina “Mwaki” (ikimaanisha moto kwa lugha ya jamii ya Kamba, ambapo alitumia picha hizo ambazo zilitengenezwa katika kipindi cha picha Tajiri kama msingi wa uchongaji, ambapo kila mmoja alihusika kukamilisha (sura zima na kuangazia usanii wote zitawakilishwa katika riporti zima”).Kuinua usanii kwa njia hii ilidhihirisha njia ya ubunifu wa kushiriki na kuangazia katika mada kutokana na warsha, na pia ikuwe ya thamani katika matokeo ya umma kwa upana Zaidi mwaka ujao.

VIDEO SHIRIKISHI

Wakati kikundi cha Nairobi kilifanyia kazi maswali ya café ya ulimwengu,Wahusika wa royal Holloway alitengeneza mbinu ya video shirikishi kuunda video mbili ziliangazia kuondelewa kwa ukoloni kwa sayansi ya moto ,mazoezi yao ya utafiti ,na mawazo yao kuhusu yale ambayo walikuwa wameyasikia tayari katika warshi. Walitilia maanani umuhimu na nguvu za uharaka watu walionazo sanasana kupitia kwa mbinu za kushirikiana, katika kufanya maamuzi yao katika utawala wa moto,lakini pia wakala ya watafiti na upendeleo wao ukiundwa na mifumo ama urithi wa kikoloni. Suala hilo la uwasilishaji wa chini wa baadhi za dunia katika kukusanya data ya kimwili iliibuliwa, Kwa mfano;uzalishaji wa data za uundaji wa mfano wa moto,na hitaji la kushughulikia mapungufu haya.

Video shirikishi ya pili iliibua maswali kadhaa kwa maongezi Zaidi-ikiwepo ni malengo yepi yaliyoko katika mifumo ya kisheria kuhusiana na moto na zinaegemea nini n ani kina nani ambao wanahusika katika mifumo ya kisheria kuhusiana na moto na zinaegemea nini na ni kina nani ambao wanahusika katika malengo haya?Nini vikundi tofauti vinahitaji kotoka kwa mandhari haya, na taratibu tofauti za moto usaidia vipi malengo hayo?;Ni taratibu gani za moto ambazo huwa tunaziona katika sheria na mitazamo ya kibinadamu katika matumizi ya moto(zinaambatana na historia ya moto katika madhara? Zinatoa moto ambao unahitajika kufanya mimea kuwa katika kiwango Fulani;Hali ya hewa inahitajika kutambuliwa katika usimamizi wa moto baadaye?) Ni jinsi gani tunaweza kushughulikia usambazaji wa manufaa nagharama tofauti, katika matumizi tofauti ya moto katika taratibu za usimamizi? Na mwisho kabisa ,ni jinsi gani taratibu za haki za moto zitakaa?

 

TAMKO LA UMOJA

Kikao cha mwisho cha warshi hiyo ilihusisha maendeleo ya tamko la Pamoja. Wahusika Nairobi walijadiliana kwa makusudi mahitaji muhimu ya usimamizi wa moto nchini Kenya,na jambo ambalo wangekubaliana awali,kuendelea suala ya usimamizi wa moto nchini.

Kikundi hiki kilitambua maendeleo ya ujumuishaji wa sera za usimamizi wa moto wa nyika,ikipeana mwelekeo katika mandhara tofauti na mifumo ikolojia ambayo inahusisha mituo ya jamii katika usimamizi wa moto kwenye mandhara,kama changamto lililo kuu kabisa.Tamko hili,ikiwa imesainiwa na wahusika wote katika nyumba inaweza pitiwa hapa

 

 

Wakati huo huo,katika warsha sambamba huko Royal Holloway,wanachama wa Leverhulme moto mwitu walikuwa wakitayarisha tamko lao la Pamoja, kwa ajili ya kuanzisha njia za usawa Zaidi za kufanya ujuzi wa moto,ambao utaandikwa kama tamko rasmi kwa kituo hicho. Maazimio ya Pamoja ni mwanzo wa safari na kujitolea kwa usimamizi bora zaidi na usawa wa moto nchini Kenya, na sayansi ya usawa zaidi ya moto mtawalia, ambayo itahitaji juhudi zinazoendelea na kufanywa upya na pande zote, ndani ya warsha na zaidi, kwa malengo ya kukutana.

 


MAWASILISHO

Katika siku ya kwanza ya warsha, tulikuwa na idadi ya mawasilisho ili kusaidia kuweka muktadha wa warsha, ikiwa ni pamoja na muhtasari wa Regimes za Moto Afrika na Prof Sally Archibald (Chuo Kikuu cha Witwatersrand), historia ya Usimamizi wa Moto katika Hifadhi ya Kitaifa ya Kruger na Terica Strydom (Hifadhi za Kitaifa za Afrika Kusini) na Kitendawili cha Moto wa nyika kilichoandikwa na Abi Croker (Chuo cha Imperial London). Hii ilifuatiwa na mawasilisho madogo kutoka kwa wanachama wa Leverhulme Wildfires kuhusu changamoto za usimamizi wa moto katika sehemu nyingine za dunia, kutoa muktadha wa kimataifa kwa masuala. Siku ya pili, pia tulikuwa na mahojiano na Harry Wright, na mwanasheria wa mazingira na mwanzilishi wa Bright Tide, kuhusu jinsi ya kushawishi sera na kuunda karatasi nyeupe (muhtasari hapa). Mawasilisho yaliyorekodiwa mapema yanapatikana ili kutazamwa hapa chini, ilhali mawasilisho ya moja kwa moja yaliyorekodiwa wakati wa warsha yatashirikiwa katika mwaka mpya.

 

 

 

Fire challenges in a Global Context – lightning presentations


Kiungo cha ripoti kamili ya warsha kitaonekana kwenye ukurasa huu mapema 2023

Asante kwa washiriki wote wa warsha kwa muda wao, shauku na kushiriki ujuzi na mawazo yao, kwa BID-C kwa uandaji, ushirikishwaji na upangaji, na kwa Taasisi ya Leverhulme Wildfires na Grantham kwa kufadhili warsha.

Wenyeviti na waandaaji: Abigail Croker, Dkt Adriana Ford, Dkt David Chiawo , Veronica Muniu, Elijah Praise, Prof Jay Mistry na Dk Cathy Smith

Wasiliana na: a.ford@imperial.ac.uk

Partners